Directorates

Mipango

Kurugenzi ya Mipango ina jukumu la shughuli muhimu zifuatazo :

Uandaaji wa mipango ya kila mwaka na mikakati kwa ajili ya matengenezo na maendeleo ya  mtandao wa barabara Kuu na Barabara za mikoa.

Kuhakikisha kuwa miundo ya uhandisi kwa ajili ya miradi ya Barabara na Madaraja yanazingatia Utaalamu maalum  kwa viwango vya kiufundi na faida za kiuchumi.

Kufanya ukusanyaji wa takwimu kwa lengo la kupanga mtandao wa barabara, miundo ya uhandisi, bajeti kwa ajili ya kazi za matengenezo, uwekezaji katika miradi ya maendeleo ya barabara, na ufuatiliaji wa maendeleo ya kazi za barabara dhidi ya malengo yaliyowekwa.

Utekelezaji wa usalama barabarani, mazingira na jamii kwa ajili ya kazi za barabara.

Kufanya upimaji wa vifaa vya ujenzi na kazi za kiraia na kuagiza utafiti juu ya vifaa vya ujenzi na teknolojia ya ujenzi kwa ajili ya kazi za barabara.

Kurugenzi ina jumla ya wafanyakazi 52 na ina Idara nne:

  • Idara ya Mipango ina jumla ya wa wafanyakazi 9  
  • Usalama Barabarani na Mazingira ina jumla ya wafanyakazi 6  
  • Ubunifu & Viwango ina jumla ya wafanyakazi  10
  • Vifaa vya & Utafiti na jumla ya wafanyakazi 27