-
Welcome
-
RAIS SAMIA AKAMILISHA UJENZI WA MIRADI YA BARABARA ILIYOASISIWA NA JPM
RAIS SAMIA AKAMILISHA UJENZI WA MIRADI YA BARABARA ILIYOASISIWA NA JPM
-
RAIS SAMIA KUFUNGUA MKOA WA RUKWA KWA MIUNDOMBINU BORA
RAIS SAMIA KUFUNGUA MKOA WA RUKWA KWA MIUNDOMBINU BORA
-
RAIS SAMIA ATOA WITO WATANZANIA KULINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA KWA MATUMIZI ENDELEVU
RAIS SAMIA ATOA WITO WATANZANIA KULINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA KWA MATUMIZI ENDELEVU
-
RAIS SAMIA AFUNGUA BARABARA YA SUMBAWANGA – MATAI – KASANGA
RAIS SAMIA AFUNGUA BARABARA YA SUMBAWANGA – MATAI – KASANGA
-
RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UKARABATI NA UPANUZI KIWANJA CHA NDEGE CHA SUMBAWANGA
RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UKARABATI NA UPANUZI KIWANJA CHA NDEGE CHA SUMBAWANGA
-
SERIKALI YAIPA TANROADS BIL. 6.5 KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL-NINO MKOANI RUKWA
SERIKALI YAIPA TANROADS BIL. 6.5 KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL-NINO MKOANI RUKWA
-
SERIKALI YAJIPANGA KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ILIYOATHIRIKA NA MVUA MKOANI RUKWA
SERIKALI YAJIPANGA KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ILIYOATHIRIKA NA MVUA MKOANI RUKWA
-
UPANUZI NA UKARABATI WA UWANJA WA NDEGE WA SUMBAWANGA UMEANZA
Serikali ya Tanzania kupitia Wakala ya Barabara Tanzania TANROADS imesaini mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni 55.908 na Kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group Co. Ltd ya China kwa ajili ya Ujenzi, upanuzi na ukarabati wa uwanja wa Ndege wa Sumbawanga mkoani Rukwa.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mradi huo kwenye ghafla iliyofanyika eneo la mradi Sumbawanga mkoani Rukwa leo April 29-2023, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa amesema Muda wa utekelezaji wa mradi huo ni miezi 18 na muda wa uangalizi (defects notification period) wa mradi ni miezi 12. 6.
Amesema kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga kwa sasa kina barabara ya kuruka na kutua Ndege ya kiwango cha changarawe yenye urefu wa meta 1,516 na upana wa meta 30, na kwamba Kupitia mradi huu, barabara hiyo itaboreshwa kufikia urefu wa meta 1,750,
Aidha upana wa meta 30 kwa kiwango cha lami na uboreshaji wa kiwanja utahusisha ujenzi wa jengo jipya la abiria, ununuzi na usimikaji wa taa za kuongozea ndege (AGL) na mitambo ya Usalama (DVOR/DME), barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani, maegesho ya magari na uzio wa usalama.
Waziri Prof: Mbarawa ametoa rai kwa viongozi na wananchi wa Rukwa kumpa Mkandarasi ushirikiano wa kutosha ili aweze kukamilisha Mradi huo kwa wakati kulingana na Mkataba huku akiwataka kusimamia ulinzi wa mradi na vifaa vitakavyotumika katika ujenzi na kusisitiza wananchi wanaozunguka eneo la mradi kuepukana na uhalifu wa namna yoyote katika mradi badala yake waulinde ili wafaidike na fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi ukiwa unaendelea hali itasaidia kulinda thamani halisi ya mradi lakini pia kukamilika kwa wakati na ubora.
Wakati huo huo Waziri Mbarawa amewaagiza Wataalam wa Wizara, TANROADS, TAA, TCAA na TMA na wadau wote kufanya kazi kwa weledi na kusimamia utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha kuwa Mradi unakamilika kwa wakati huku pia akitoa wito kwa Mkandarasi na Mhandisi Mshauri kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu ili kazi zikamilike ndani ya muda kwa viwango na gharama zilizokubalika.
Awali akitoa taarifa ya Mradi huo Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila ameishukukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi ambavyo imetoa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu inayosimamiwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
"Natoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutoa fedha za utekelezaji wa mradi huu, Mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Rukwa ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri wa anga na usafirishaji" alisema Mhandisi Mativila
Amesema kiwanja hicho cha Ndege cha Sumbawanga ni moja kati ya viwanja vya ndege muhimu nchini kinachounganisha mkoa huo na Ukanda wa Magharibi na mikoa mingine nchini pamoja na nchi jirani ambapo Uboreshaji wa miundombinu ya kiwanja hicho utachochea shughuli za kiuchumi kama vile utalii, uwekezaji, uvuvi, usafirishaji wa mizigo na abiria na shughuli za kijamii kwa ujumla.
Ameongeza kuwa Utekelezaji wa Mradi huu unagharamiwa na mkopo kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na kwamba awamu ya kwanza ya Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Kiwanja hicho ulifanywa na kampuni ya Sir Fredrick Snow & Partners Ltd ya Uingereza ikishirikiana na Kampuni ya Belva Consult ya Tanzania kati ya mwaka 2007 mpaka mwaka 2009 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania.
Amesisitiza pamoja na mambo mengine usanifu umezingatia vigezo vifuatavyo, Ujenzi wa jengo jipya la abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria 150,000 kwa mwaka, Jengo hilo litakuwa na kiota cha waongoza ndege (Air Traffic Control Cabin) juu yake, Ununuzi na usimikaji wa taa za kuongozea Ndege na mitambo ya usalama (AGL na DVOR/DME) Ujenzi wa barabara ya kuingia kiwanjani pamoja na maegesho ya magari.