• Welcome

  • WASANIFU MIRADI YA UJENZI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

    Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ameyataka makampuni yanayopewa kazi na Serikali ya kusanifu ujenzi wa barabara kufanya kazi hiyo kwa umakini kwa kutambua na kubainisha changamoto zitakazosababisha ucheleweshaji wa ujenzi wa miundombinu hiyo hapa nchini.