-
Welcome
-
TANROADS YATEKELEZA AGIZO LA BASHUNGWA, YAFUNGA MIZANI KUPIMA UZITO WA MAGARI - TUNDUMA
TANROADS YATEKELEZA AGIZO LA BASHUNGWA, YAFUNGA MIZANI KUPIMA UZITO WA MAGARI - TUNDUMA
-
MIRADI YA MIUNDOMBINU WILAYANI ILEJE KUKAMILIKA KWA WAKATI: KASEKENYA
MIRADI YA MIUNDOMBINU WILAYANI ILEJE KUKAMILIKA KWA WAKATI: KASEKENYA
-
“SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MTANDAO WA BARABARA MKOANI SONGWE”
“SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MTANDAO WA BARABARA MKOANI SONGWE”
-
SERIKALI YADHAMIRIA KUJENGA BARABARA YA RUANDA HADI ITUMBA KM 79 KWA KIWANGO CHA LAMI
SERIKALI YADHAMIRIA KUJENGA BARABARA YA RUANDA HADI ITUMBA KM 79 KWA KIWANGO CHA LAMI
-
RC CHONGOLO AIPA HEKO TANROADS, BIL 5.7 ZATOLEWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU MKOANI SONGWE
RC CHONGOLO AIPA HEKO TANROADS, BIL 5.7 ZATOLEWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU MKOANI SONGWE
-
TANROADS yakamilisha ujenzi wa Jengo la abiria Kiwanja cha Ndege cha Songwe
TANROADS yakamilisha ujenzi wa Jengo la abiria Kiwanja cha Ndege cha Songwe
-
Serikali kuifungua Songwe kwa miradi 9 ya kimkakati ya barabara na madaraja
Serikali kuifungua Songwe kwa miradi 9 ya kimkakati ya barabara na madaraja
-
MIUNDOMBINU YA MKOA WA SONGWE YAZIDI KUBORESHWA NA SERIKALI
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Songwe imekamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kipande cha mita 500 katika Mji wa Chitete Makao Makuu ya Wilaya ya Momba ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali kila Makao Makuu ya wilaya lazima miundiombinu iboreshwe.
Msimamizi wa kitengo cha matengenezo ya barabara mkoa wa Songwe Mhandisi Silvan Henry Mloka amebainisha hayo Agosti 3, 2023 alipozungumza na kipindi cha TANROADS mkoa kwa Mkoa kwa niaba ya Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga.
Amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 kiasi cha fedha shilingi milioni 500 kilitengwa na Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami, kuweka taa za barabarani, pamoja kujenga Makalavati kwa ajili ya njia za Maingilio.
Mhandisi Mloka amesema mradi huo umetekelezwa na Mkandarasi mzawa wa kampuni ya GNMS CONTRACTORS CO LIMITED ya Iringa, ambapo barabara hiyo ya lami ni mwanzo wa kuendeleza na kuupendezesha mji kwa ujenzi wa miundombinu bora, na kwamba kila mwaka wa fedha Serikali itaendelea kutenga na kutoa fedha kwa ajili kujenga barabara za lami mpaka hapo Mji wote wa Chitete utakapozungukwa na lami hasa katika barabara zote ambazo zinahudumiwa na TANROADS.
"Tunaishukuru na kuipongeza Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga na kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara pamoja na madaraja, vilevile tunamshukuru Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa ambaye mara zote anasisitiza na kutusimamia kwamba kazi zifanyike vizuri kwa ueledi, pia Mtendaji wetu Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta ambaye naye anatusisitiza kuchapa kazi kwa bidii na kusimamia vema kiasi cha fedha kinachotolewa na Serikali ili kitumike vizuri kama inavyopaswa kwa kuzingatia thamani ya fedha na miradi kujengwa kwa viwango vinavyokubalika kwa maslahi ya Umma" ameongeza Mhandisi Silvan Mloka.
Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Chitete yalipo Makao Makuu ya wilaya ya Momba Ruben Silvester Pazia amesema "tunampongeza sana, Rais wetu Dkt. Samia kwa kuweza kusaidia ujenzi wa kipande hiki cha barabara, pamoja na kazi kubwa anayofanya, tunamuomba atuongezee barabara nyingine za lami ili Wananchi waweze kupata huduma ya usafiri wa uhakika na hivyo kusafirisha mazao ya chakula kwa urahisi, kupunguza gharama na muda wa safari.
Aidha Mchungaji Erasto L Siwiti wa kanisani la FPCT Chetete ameishukukuru na kuipongeza Serikali kwa Jitihada mbalimbali inazofanya kusogeza huduma ya usafiri wa barabara za lami karibu zaidi na Wananchi huku akitoa ombi kwa Rais Dkt Samia na Watendaji wake kuendelea na jitihada zaidi za ujenzi wa miundombinu hiyo hasa maeneo ya Vijiji ili Wananchi ambao ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula wapate urahisi wa kusafirisha na kuuza mazao yao kwenda kwa walaji na hivyo kujipatia kipato.
Wakizungumza kwa niaba ya Wananchi wenzao Bwana Stefano Simsimba, Fulgence Patrick, Enock Mwasanya, Julius Mwasoso Mgogo na Filisian Johane wote wakazi wa wilaya ya Momba wametoa pongeza nyingi kwa Rais Dkt. Samia kwa kuwakumbuka na kuanza kuwapatia barabara za lami.
Wameongeza kuwa" tumepokea kipande hiki cha barabara ya lami kwa furaha kubwa sana, mwanzo hatukuwahi kuiona lakini kwenye utawala wa Rais Dkt. Samia ndio tumeona hii lami hapa, tunamuomba aendele kutuongeza barabara nyingi zaidi za lami katika Wilaya yetu ya Momba ili tuweze kuongeza kipato katika shughuli za uzalishaji hasa pale tunaposafisha mazao yetu kwa haraka kwenda sokoni kwa kuzingatia tupo jirani na Nchi ya Zambia kibiashara hii ni fursa kwetu"